Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa na utapiamlo vinaweza kutokomezwa: Ban

Njaa na utapiamlo vinaweza kutokomezwa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kwamba ulimwengu unaweza kutokomeza njaa na utapiamlo kwa sera nzuri na uwekezaji wenye busara.

Bwana Ban amesema hayo wakati wa kufunga kikao cha mashauriano ya ngazi ya juu kuhusu njaa, usalama wa chakula na lishe katika muktadha wa maendeleo baada ya mwaka 2015, ambacho kimemalizika leo mjini Madrid, Uhispania.

Amesema nchi nyingi ambazo zinaibuka kutoka kwa umaskini kama vile Brazil, Uchina na India, zinaelewa kuwa kuwa na usalama wa chakula kunaweza kufungua milango ya ukuaji, na kwamba kilimo katika maeneo ya vijijini kinaweza kupunguza umaskini, na kwa hivyo zimekifanya suala la kipaumbele

Amesema saa chache kabla kuanza kuhesabu siku elfu moja hadi tarehe ya kufikia malengo ya milenia, juhudi zaidi zinatakiwa kufanywa, kwani kutokomeza njaa si jambo rahisi.