Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani Afrika kuendelea kumulikwa ndani ya Baraza : Rwanda

Amani Afrika kuendelea kumulikwa ndani ya Baraza : Rwanda

Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi Aprili Balozi Eugène-Richard Gasana ametangaza mpango kazi wakati wa kipindi chake cha mwezi huu wa Aprili ambapo miongoni mwa mambo yatakayomulikwa ni jinsi ya kuzuia migogoro barani Afrika.  Balozi Gasana ambaye ni Mwakilishi wa kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa amewaeleza waandishi wa habari kuwa suala hilo litaangaziwa wakati wa kikao cha ngazi ya mawaziri  tarehe 15 mwezi huu kikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Rwanda. Masuala mengine yatakayoangaziwa wakati wa kipindi chaRwandani ukatili wa kingono kwenye migogoro na hali ya amani hukoMali, Jamhuri ya Afrika ya Kati,SyrianaYemenambapo pia mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa nchi za Maziwa Makuu Mary Robinson anatarajiwa kuwasilisha ripoti mbele ya Baraza la Usalama.

 Katika kikao hicho Balozi Gasana aliulizwa kuhusu madai kuwa azimio lililopitishwa wiki iliyopita la kuipatia ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO uwezo wa kushambulia ushindi juu ya nchi yake.

 (SAUTI YA Balozi Gasana)

 “Ni ushindi nafikiri siyo tu kwa Congo au nani, bali ni ushindi kwa wapenda amani wote kwenye eneo hilo. Katika hilo mimi kwa nafasi yangu ya Urais wa Baraza la Usalama na pia mwakilishi wa Rwanda, niseme ni ushindi kwetu sote.Bila shaka FDLR na ilani zao za kikabila bado wanajaribu kutishia Rwanda, kuleta ilani zao, kuua watu kila mahali Rwanda, Congo. Tunazungumzia vitendo vya ubakaji. Tunaamini kuwa baraza litashinikiza zaidi ili kutokemeza vikundi hivyo kutoka Congo, kwa sababu wananchi Congo wanateseka, halikadhalika, Rwanda. Hatupaswi kuangalia tu bali tunapaswa kuchukua hatua.”