Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yawezeshwa kusaidia wakimbizi Uganda

WFP yawezeshwa kusaidia wakimbizi Uganda

Serikali ya Brazil hii imetoa mchango wake wa kwanza kwa shirika chakula na kilimo duniani, FAO nchini Uganda ambapo tani 2000 za mchele zenye gharama ya dola Milioni moja zilizitolewa. Mchele huo utatumiwa miezi inayokuja kuwasaidia wakimbizi 155,000. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA JASON)

Mjumbe wa masuala ya Brazil nchini Uganda Antonia Ricarte amesema kuwa taifa lake limeridhishwa na hatua ya kuwasiadia wakimbizi walio nchini Uganda. Ricarte amesema kuwa Brazil imekuwa mfadhili mkubwa kwa Shirika la WFP duniani na tangu mwaka 2011 taifa hilo limetoa mchango wa tani 300,000 za nafaka kwa nchi 35 zilizo na tatizo la usalama wa chakula. Amesema kuwa Brazil imeongeza mchango wake kutoka dola milioni moja mwaka 2007 hadi dola milioni 82 mwaka 2012. WFP imeelezea shukrani zake kwa serikali ya Brazil kwa msaada wake kwa kuwa msaada huo utatumika kuwasaidia wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo walio nchini Uganda. Kwa sasa WFP inawashughulikia takriban wakimbizi 155,000 pamoja na kuwapa lishe watoto walio na utapiamlo. Msaada huo unajumuisha nafaka, mafuta ya kupikia na chumvi vyote vikitolewa kweneye vituo  nane nchini Uganda.