Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unicef yapiga kambi Niger kukabiliana na utapiamlo

Unicef yapiga kambi Niger kukabiliana na utapiamlo

Mapigano yanayoendelea nchini Mali yamesababisha zaidi ya wakazi 270,000 wa nchi hiyo iliyoko Magharibi mwa Afrika kukimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi. Hata hivyo wakiwa njiani wanakumbana na kadhia mbalimbali na watoto wa wanawake huathirika zaidi.  Nchini Niger, ambako yanapokelewa makundi ya wakimbizi kutoka Mali, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelazimika kupiga kambi humo kusaidia kwa matibabu kutokana na magonjwa kadhaa, ukiwemo utapiamlo unaotokana na lishe duni. Basi kupata undani wa ripoti hiyo ungana na Joseph Msami.