Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mary Robinson awa Mwakilishi wa Ban kwa nchi za Maziwa Makuu

Mary Robinson awa Mwakilishi wa Ban kwa nchi za Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Mkuu wa zamani wa tume ya haki za binadamu ya Umoja huo , Mary Robinson kuwa Mwakilishi wake maalum kwa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika.  Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bi. Robinson atakuwa na dhima ya msingi ya kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya amani, ulinzi na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC.  Kabla ya kuwa kamishna wa haki za binadamu kati ya mwaka 1997 hadi 2002, Bi. Robinson alikuwa Rais wa Ireland kuanzia mwaka 1990 hadi 1997.