Pakistan yapinga matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani nchini mwake.

15 Machi 2013

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu vita dhidi ya ugaidi na haki za binadanmu Ben Emmerson amehitimisha mikutano yake nchini Islamabad, Pakistani kuhusu matumizi ya vifaa vya anga visivyo na rubani ambapo kwa ujumla amesema wapakistani wanapinga matumizi ya vifaa hivyo.  Katika taarifa yake aliyoitoa baada ya mikutano hiyo iliyofanyika kati ya tarehe 11 na 13 mwezi huu huko Islamabad, Emmerson amesema Pakistani hairidhii hatua ya Marekani kutumia vifaa hivyo kwenye eneo lake na inaona kitendo hicho kama ukiukwaji wa utaifa na uhuru wa Pakistani.  Amesema Pakistan imetoa wito kwa taifa la Marekani kusitisha kampeni hiyo mara moja  na imepinga madai kuwa imeshindwa kukabilina na ugaidi nchini mwake.

Kwa mujibu wa Emmerson, Pakistani inalenga kuwa na mkakati endelevu wa kudhibiti ugaidi ambao utahusisha mashauriano kwenye ukanda huo na ambao siyo tu utadhibiti uendelezaji wa ugaidi bali pia utashughulikia chanzo chake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter