Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yazidi kuhatarisha wakimbizi Jamhuri ya Afrika ya kati: UNHCR

Mapigano yazidi kuhatarisha wakimbizi Jamhuri ya Afrika ya kati: UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali iliyopo  kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo uvamizi wa juma lililopita umeyaweka hatarini maisha ya raia wakiwemo wakimbizi kutoka  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC.  UNHCR inasema kuwa waasi wa Seleka waliotia sahihi makubalino ya amani na serikali miezi miwili iliyopita waliuvamia na kuutwaa mji wa Bangassaou. Waasi hao wamekuwa wakisonga kuelekea mashariki  kwenda mji wa Zemio ambapo wakimbizi 3,300 kutoka mkoa wa Orientale nchini DRC wamepiga kambi. Mapigano ya tangu mwezi Disemba kati ya wapiganaji wa Seleka na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati yamezua madhara kwa karibu wakimbizi 5300 na wengine wa ndanbi 175,000.

Fatoumata Lejeune-Kaba ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA Fatoumata)