Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya hatari inayokodolea macho Mashariki ya Kati

UNHCR yaonya hatari inayokodolea macho Mashariki ya Kati

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres amerejelea wito wake kwa serikali akizitaka kutenga fedha za kuwasaidia wakimbizi wa Syria na nchi zilizowapa makao. Guterres ameonya kuwa ikiwa fedha za kuwasaidia wakimbizi wa Syria hazitakuwepo, msaada kwa wakimbizi hao utakosekana hali ambayo itazua msukosuko katika eneo hilo. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA JASON)

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beirut ikiwa ni miwili tangu kuanza kwa mzozo nchini Syria, Bwana Guterres amesema kuwa kusambaa kwa mzozo huo na mateso wanayopitia wananchi wa Syria na makubwa. Amesema kuwa pengo la mahitaji na huduma zilizopo linazidi kuwa kubwa akiongeza kuwa hakuna vile pengo hilo linaweza kuzibwa na bajeti za sasa. Ameonya kuwa iwapo mapigano hayatasitishwa eneo zima la mashariki ya kati litaathiriwa. Kulingana na Guterres kuna pengo la dola milioni 700 na hadi sasa  mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yatapokea tu asilimia 30 ya fedha hizo zinazohitajika kutoa mahitaji muhimu kwa zaidi ya wakimbizi milioni moja. Ameelezea matumaini yake kuwa ahadi ya fedha zilizotolewa mwezi Januari kwenye mkutano uliondaliwa nchini Kuwait zinatolewa ili kugharamia huduma za Umoja wa Mataifa.