Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga yatokanayo na maji yanaathiri kila nchi: Jeremić

Majanga yatokanayo na maji yanaathiri kila nchi: Jeremić

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremić amesema majanga yatokanayo na maji yameendelea kusababisha madhara kwa nchi mbali mbali duniani, ziwe maskini au tajiri huku akiweka bayana kuwa nchi maskini zinabeba mzigo zaidi wakati wa kukabiliana na hali hiyo.

Akizungumza katika kikao maalum cha baraza hilo kuhusu majanga yatokanayo na maji, Bwana Jeremić amesema ni miezi minne tu iliyopita kimbunga Sandy kilipiga maeneo ya Caribbean na Amerika Kaskazini na kusababisha vifo vya watu takribani Mia Mbili na uharibifu wa mali huku maelfu ya watu katika nchi maskini na zile tajiri wakiendelea kujikwamua kutokana na madhara ya kimbunga hicho.

Amegusia nchi za Kusini mwa Afrika ambako amesema madhara ya mafuriko yameendelea na kuharibu mazao na wananchi wakikwapuliwa uwezo wao wa kuishi kwa kiasi kikubwa. Rais huyo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akatanabaisha zaidi.

(SAUTI YA Jeremić)