Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latakiwa kuruhusu jeshi la kulinda amani Drc Kongo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latakiwa kuruhusu jeshi la kulinda amani Drc Kongo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kuruhusu jeshi la kulinda amani ili kusaidia kurejesha hali ya utulivu Mashraiki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Huo ni wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon wakati akihutubia baraza hilo mapema Jumanne. Amesema hali katika eneo hilo ni mbaya ambapo maelfu ya raia wameyakimbia makazi yao kufuatai mapigano kati ya jeshi la serikali na majeshi ya waasi.

Bwana Ban amesema jeshi hilo litahakikisha malengo yanatimizwa kufuatia mkataba wa  amani na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliotiwa saini na viongozi kadhaa wa Afrika February 24 mwaka huu mjini Adis Ababa Ethiopia..

Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema hatua hiyo itawezesha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Kongo (MONUSCO) kujisimamia wenyewe na kufanikisha kurejesha amani hata kama majeshi ya nchi hiyo hatatakuwa na ujumbe huo bega kwa bega.

SAUTI YA BAN

‘Utekelazaji huu ambao awali ulihitajika na viongozi wa kanda unalenga kuondoa kwa haraka tishio la ghasia na kusaidia ujumbe wa Umoja wa Mataifa ambao umekuwa katika operesheni hiyo kwa muda mrefu.Jeshi hili litafanya kazi ya kuviweka pamoja vikundi pinzani na kuifikia nchi nzima huku vikisaidia kumaliza mapigano kwa vikundi hivyo .Kazi hii inahitaji jeshi lenye nguvu ili kulinda amani’’.

Bwana Ban amesema mazungumzo baina ya nchi zilizoshoriki kutuma majesh kusaidiana na MONUSCO lakini hatua hiyo itategemea kukubalika kwa swala hilo katika Barza la Usalama la Umoja wa Mataifa.