Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la wanawake 10 kupanda Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania:WFP

Kundi la wanawake 10 kupanda Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania:WFP

Kundi la wanawake saba raia wa Nepal ambalo lina sifa ya kuukwea mlima mrefu zaidi duniani  wa Everest na milima mingine barani Ulaya na nchini Australia sasa limeungana na wanawake wengine watatu wenye asili ya Afrika kuukwea mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari yao ya kuukwea mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 itaanzia kwenye mji wa Moshi ulio kaskazini mwa Tanzanzia kesho Jumatano. Shughuli hiyo inafadhiliwa na wizara ya utalii na maliasili nchini Tanzania, mbuga za kitaifa nchini Tanzania pamoja na Shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Kati ya wanoukwea mlima kilimnjaro ni Ashura Kayupayupa ambaye ni mwanaharakati wa kupinga ndoa za mapema na mwalimu Anna Philipo Indaya  kutoka jamii ndogo ya Hadazabe nchjini Tanziania. Wote hao wataungana na balozi anayepinga njaa wa Shirika ma mpango wa chakula duniani WFP Hlubi Mboya ambaye ni mmjoa wa wasanii maarufu zaidi  kusini mwa Afrika.