Skip to main content

Watu wa asili wanastahili kuwa na mipango kulingana na tamaduni zao:UM

Watu wa asili wanastahili kuwa na mipango kulingana na tamaduni zao:UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uhuru wa haki za binadamu za watu wa asili amesema kuwa watu wa asili wanastahili kuwa na mipangilio yao ya uongozi ili kuhakikisha kuwa inaambatana na tamaduni zao.

Kupitia kwa ripoti yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa James Anaya amesema kuwa sera na miradi mingine iliyo na lengo la maendeleo ya kiuchumi inaweza kuwaathiri watu wa asili. Anaya amesema kuwa hata kama miradi ya kimaaendeleo inawaathiri watu wa asili mara nyingi huwa inatekelezwa bila ya kuomba ushauri nao au bila ya wao kuruhusu.

Mjumbe huyo ametoa wito kwa watu wa asili kupewa elimu ya kutosha ili kuwawesesha kushiriki vilivyo kwenye miradi ya maendeleo inayowaathiri. Anaya amewashauri watu wa asili kusimamia na kuongoza masuala yao na kushiriki vilivyo katika maamuzi yanayowaathiri na kushirikiana vilivyo na serikali katika nyanja zote.