Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM asema mageuzi hayakwepeki ndani Umoja huo

Rais wa Baraza Kuu la UM asema mageuzi hayakwepeki ndani Umoja huo

Vyombo muhimu vya Umoja wa Mataifa ikiwemo baraza la usalama, vinapaswa kufanya mageuzi ili kuleta nguvu na ushawishi muhimu katika enzi hii ya karne ya 21.Hayo ni kwa mujibu wa rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Joseph Deiss ambaye ameonya kuwa utendaji wa umoja huo wa mataifa kwenye enzi hii mpya hauwezi kuleta tija kama kutakosekana mageuzi ya kweli kwenye vyombo hivyo muhimu.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake nchini Chile Bwana Deiss alianisha nafasi ya Umoja wa Mataifa katika amani ya ulimwengu akisema kuwa chombo hicho kimbilio la watu kwani kinabeba sura ya mafungamano toka pembe zote za dunia.