Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar imeendelea kupiga hatua kutekeleza mageuzi- Mtaalamu UM

Myanmar imeendelea kupiga hatua kutekeleza mageuzi- Mtaalamu UM

Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar amesema nchi hiyo imeanza kupiga hatua kwa kuchomoza mifumo inayozingatia misingi ya haki za binadamu lakini ameonya kuwa safari bado ni ndefu.

Toma’s Ojea amesema kuwa taifa hilo linapiga hatua kusonga mbele na kukaribisha matumaini ambayo amesema kuwa yanafungua ukusara mpya na hivyo kuna umuhimu wa kuungwa mkono.

Ametoa kauli hiyo baada ya kuhitimisha ziara nchini humo ambapo alitembelea maeneo kadhaa ikiwemo majimbo ya Rakhine na Kachin ambayo mwaka jana yalikubwa na majanga na migogoro iliyotokana na mapigano ya kikabila ma mafuriko.

Hata hivyo ameitolea mwito serikali kuchukua hatua mujarabu kutatua mikwamo ya hapa na pale ambayo bado inakwaza misingi ya haki za binadamu.

Mtaalamu huyo anatazamia kuwasilisha ripoti yake kwenye kikao cha baraza la haki za binadamu kilichopanga kuanza kukutana tarehe 11 mwezi ujao.