Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaanza kusambaza dawa za kutakasa maji kwa Wasyria

UNICEF yaanza kusambaza dawa za kutakasa maji kwa Wasyria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeanza operesheni ya aina yake ya kuhakikisha wasyria walioko katika mzozo wanapata majisafina salama kwa kusambaza dawa za kutakasa maji.

Matenki yaliyojazwa maji ambayo yamewekewa dawa maalumu za kutakasa maji yamesafirishwa kupitia mpaka waJordanhadi katika miji yaHoms,Aleppo,Hamana Idlepo ambako kiasi cha watu zaidi ya milioni 10 wapo kwenye hali mbaya.

UNICEF inakadiria kuwa katika kipindi cha wiki chache zijazo, itakuwa imesafirisha maji tani 1,000 katika zaidi ya majimbo 14 nchini humo. Taarifa zaidi na George Njogopa

(SAUTI YA GEORGE)