Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Syria, raia taabani: OCHA

Mzozo wa Syria, raia taabani: OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu  misaada ya kibinadamu OCHA inasema raia wa Syria ndio wanaingia gharama kutokana na mzozo unaoendelea nchini mwao.  OCHA inasema mzozo huo umefanya watu kupoteza tegemeo lao la maisha, kazi, nyumba, chakula, maji huku wakishuhudia maisha ya baadaye ya watoto wao yakizidi kuhatarishwa. Halikadhalika nyumba, viwanda mitandao ya simu, barabara, madaraja, shule na sekta za mafuta na kilimo vyote vimeharibiwa.  Jens Laerke ni msemaji wa OCHA na ametoa taarifa akimkariri mratibu wa ofisi hiyo huko Mashariki ya Kati.

(SAUTI YA Jens)

 “Amegusia tena uhaba mkubwa wa fedha kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na kwa sababu  hiyo amesema kutoka na uhaba hawawezi kulisha wanaohitaji chakula, kutibu wagonjwa na hata kutoa makazi kwa familia zenye mahitaji. Hata hivyo amesema suluhisho la mzozo siyo la kibinadamu bali linaweza kutatuliwa kupitia wanasiasa na watoa maamuzi.”