Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye msafara wa UNHCR waingia kaskazini mwa Syria

Hatimaye msafara wa UNHCR waingia kaskazini mwa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, kwa mara ya kwanza limefaulu kusambaza vifaa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya baridi kwa wakimbizi wa ndani wa Syria waliotawanyika katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Vifaa hivyo ni pamoja na mahema, mablanketi ambapo usambazaji wa huduma hizo ulifanyika kwa ufanisi mkubwa na hii ni kutokana na maandalizi mazuri yaliyoweka na pande zote zilizohusika ikiwemo shirika la mwezi mwekundu la Syria, serikali na usharika wa kitaifa wa Syria.

Yacoub Elhilo ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Kati ya UNHCR kwenye ofisi ya Afrika kaskazini.

(CLIP Yacoub Elhilo)

“Kwa UNHCR hii ni  mara ya kwanza kwa wafanyakazi wake wa kigeni na wale wa ndani kusafiri na kuingia hadi maeneo ya ndani  kabisa ya Kaskazini Magharibi  ya Syria  kusambaza misaada. Yaani walisafiri kabisa licha ya kwamba mazingira ni magumu ambayo siwezi kuelezea lakini waliweza kusambaza misaada. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa UNHCR na pengine kwa Umoja wa Mataifa kupeleka wafanyakazi wake wa ndani na wan je kwenye maeneo hayo kutoka ndani ya nchi.”

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wakimbizi wanaomiminika katika nchi jirani na Syria kutokana na machafuko yanayoendelea kuchacha nchini Syria. Ripoti zinasema kuwa idadi yao mpaka juma hili ilifikia  wakimbizi  728,553 ambao tayari walikuwa wameandikishwa