Kitabu cha Annan chamulika changamoto na mafanikio

14 Januari 2013

Masuala ya amani, ulinzi, usalama, uongozi bora na misaada na maendeleo ni miongoni mwa mambo yaliyochukua nafasi katika kitabu kilichoandikwa na Katibu Mkuu  mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, A Life in War and Peace.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kitabu hicho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani hii leo, Bwana Annan amesema alijisikia kuandika kitabu hicho ili kuonyesha changamoto, mafanikio aliyopata wakati akihudumu nafasi ya Katibu Mkuu.

Amesema kupitia kitabu hicho watu wanaweza kufahamu jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi ikiwemo jitihada za Umoja huo kuleta amani.

“Suala nyingine ambalo nimegusa katika kitabu changu ni bara la Afrika na kazi inayofanywa na UM barani humo. Katika kulinda amani, suala la msaada wa kibindamu, utawala wa sheria na changamoto ambazo tumekuwa nazo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Afrika. Nimeandika pia kuhusu athari zitokanazo na mapambano kwa ajili ya uhuru, juu ya utawala wa sheria.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter