Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapinduzi ya teknolojia ya simu yachochea maendeleo ya huduma za kijamii

Mapinduzi ya teknolojia ya simu yachochea maendeleo ya huduma za kijamii

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii duniain kote ikiwemo nchi zinazoendelea. Inaelezwa kuwa matumizi ya simu ikiwemo zile za mkononi ambazo kwa sasa zinaweza kutuma picha na hata sauti, zimeweza kuwa mkombozi kwa mwananchi wa kawaida.

Mathalani wapo waliofungua vioski kwa ajili ya kutoa huduma za kutuma pesa kwa kutumia simu, na hata wengine wanapata huduma za kitabibu kupitia simu za mkononi. Maendeleo hayo na changamoto zitokanazo na mafanikio hayo ni miongoni mwa masuala yaliyoibuka kwenye mkutanowa kimatifa wa shirika la mawasiliano ya simu duniani, ITU huko Dubai, Falme za kiarabu. Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania Profesa John Nkoma anayehudhuria mkutano huo kuhusu maendeleo yatokanayo na mapinduzi ya sekta ya mawasiliano ya simu.