Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira zaidi ya wanaume: ILO

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira zaidi ya wanaume: ILO

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira kwa viwango vikubwa zaidi ya wanaume kote duniani, huku matarajio ya hali hiyo kurekebishwa yakiwa adimu katika miaka ijayo, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Ajira Duniani, ILO.

Ripoti hiyo ya ILO kuhusu mienendo ya kimataifa kuhusu wanawake mwaka 2012, inaangalia mapengo yaliyopo ya kijinsia katika nafasi za ajira, ukosefu wa ajira, ushirikishaji wa wafanyakazi, hatari zilizopo na ubaguzi katika sekta za ajira na uchumi.

Kote duniani, kabla ya mdororo wa kiuchumi, mapengo haya ya viwango vya ajira na ukosefu wa ajira yalikuwa yanaelekea kuzibwa, kwa mujibu wa ILO. Mdororo wa kicuchumi ulibadili mkondo huo katika maeneo yaloathiriwa zaidi duniani.