Ban azindua mkakati mpya wa kulifikia lengo la maendeleo ya milenia kuhusu elimu

26 Septemba 2012

Ahadi za zaidi ya dola bilioni 1.5 zimetolewa leo kwa ajili ya kuufadhili mkakati mpya wa kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya kwenda shule, wa Elimu Kwanza, au Education First. Mkakati huo ambao umezinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, una shabaha ya kuuchagiza ulimwengu kulifikia lengo la milenia la elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Bwana Ban ameelezea elimu kama kitu cha kuaziziwa katika maendeleo.

“Elimu ni sehemu ya ujenzi wa kila jamii, na njia ya kuondoka katika umaskini. Elimu zaidi inamaanisha uwezo wa kukabiliana na umaskini na njaa, na nafasi zaidi kwa wanawake na wasichana, afya zaidi, usafi zaidi, nguvu zaidi za kukabiliana na HIV, malaria, kipindupindu na maradhi mengine yanayoua. Kupiga hatua katika elimu kunaleta kupiga hatua katika malengo yote ya maendeleo ya milenia.”

Makapuni kadhaa na wakf za kibinafsi zimeunga mkono mkakati wa Elimu Kwanza. Mataiofa binafsi pia yamefanya ahadi, yakiwemo Australia, Bangladesh, Afrika Kusini, Timor-Leste na Denmark

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter