Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu ni muhimu kwa uchumi na maendeleo:FAO

Misitu ni muhimu kwa uchumi na maendeleo:FAO

Katibu mkuu wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Jose Graziano da Silva amesistiza umuhimu wa misitu kwenye maendelo endelevu. Akifungua mkutano wa siku tano wa kamati ya misitu ya FAO, da Silva amesema kuwa uhusinao kati ya misitu na maendeleo endelevu ni kati ya masuala yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa RIO+20 mwezi Juni. Amesema kuwa misitu inayochukua asilimia 31 ya dunia ina wajibu mkubwa kwenye uchumi wa kitaifa na kimataifa na kwenye mikakati ya FAO ya kupunguza njaa, utapiamlo na umaskini.

Karibu watu milioni 350 kati ya wale maskini zaidi duniani wakiwemo watu milioni 60 wa asili wanategemea misitu kwenye mahitaji yao ya kila siku lakini hata hivyo kwenye mataifa mengi uharibifu wa misitu unachangia kuwepo athari zikiwemo mmomonyoko wa udongo kila mwaka.