Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warsha ya wanafunzi wanaoandaa mijadala inayoiga UM yakamilika mjini New York

Warsha ya wanafunzi wanaoandaa mijadala inayoiga UM yakamilika mjini New York

Warsha ya kuelimisha wanafunzi na walimu kuhusu jinsi shughuli za Umoja wa Mataifa zinavyoendeshwa imekamilika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Warsha hiyo ya siku tatu, iliandaliwa na idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuelimisha watu kuhusu jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi, na imewaleta pamoja wanafunzi 50 na walimu 20 kutoka nchi 27 tofauti, ambao hujihusisha na kuandaa mijadala ambayo inaiga mtindo wa Umoja wa Mataifa wa kujadili masuala tofauti tofauti yanayoathiri ulimwengu mzima.

Katika mahojiano na Radio ya UM, mwanafunzi Monica Akech kutoka chuo kikuu cha Cavendish kilichoko nchini Uganda, ameniambia ni nini alichoiga kutoka kwenye warsha hiyo.

(SAUIT YA MONICA AKECH)