Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame unaojirudia ni ishara ya haja ya kudhibiti rasilimali ya maji na kulinda usalama wa chakula

Ukame unaojirudia ni ishara ya haja ya kudhibiti rasilimali ya maji na kulinda usalama wa chakula

Ukame katika baadhi ya maeneo duniani umeathiri uzalishaji wa chakula na kuchangia kupanda kwa gharama za chakula kila mwaka tangu mwaka 2007, ikiashiria haja ya kubadili jinsi maji yanavyotumika na kupotea katika mfumo mzima wa uzalishaji wa chakula.

Huu ni moja ya ujumbe maalumu uliotolewa na shirika la kilimo na chakula FAO wiki hii katika wiki ya maji duniani inayofanyika mjini Stockholm Sweeden. Hafla hiyo ya kila mwaka inawaleta pamoja watunga sera na wataalamu kutoka kila pembe ya dunia ili kukutana na kujadili masuala muhimu yahusuyo maji na udhibiti wa bidhaa hiyio hadimu. Maelezo zaidi na George Njogopa.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)