Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasisitiza Umuhimu wa Diplomasia ya Kuzuia Migogoro

Baraza la Usalama lasisitiza Umuhimu wa Diplomasia ya Kuzuia Migogoro

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea umuhimu wa diplomasia ya kutambua mapema na kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani kama njia ya kuzuia migogoro zaidi. Wanachama wa Baraza hilo wameelezea umuhimu wa kisiasa, kibinadamu na kimaadili, pamoja na faida za kiuchumi za kuzuia kutokea, kuongezeka au kurejelea migogoro.

Katika taarifa ilotolewa kwa waandishi wa habari baada ya kuelezewa kuhusu kazi ya Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Diplomasia ya Kuzuia migogoro katika Asia ya Kati, wanachama Baraza la Usalama wametaja kituo hicho cha kikanda kama mfano wa chombo mojawepo cha Umoja wa Mataifa cha kuzuia migogoro, na hivyo kukipongeza kwa juhudi zake katika kuyasaidia mataifa ya Asia ya Kati kukabiliana na matishio ya kitaifa na ya kimataifa kwa amani na maendeleo endelevu ya kanda hilo.