Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa Huduma ya Kujitolea

Katika Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa Huduma ya Kujitolea

Kwa muda wa miaka 67, Nelson Mandela alijitolea kuhudumia ubinadamu kama wakili wa haki za binadamu, kama mfungwa kwa ajili ya dhana yake, mshauri wa amani wa kimataifa, na rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia katika taifa huru la Afrika Kusini.

Kila mwaka Julai kumi na nane, tangu mwaka 2010, watu binafsi kote ulimwenguni wanahimizwa kujitolea kwa muda wa dakika 67 kuwahudumia wengine bila malipo, kwa heshima ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya Nelson Mandela. Na katika ujumbe wake kupitia kwa video, Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon ametoa wito watu watoe huduma ya kujitolea

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katika kuutimiza ujumbe huu, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu mjini New York, leo wamejitolea kupika na kuwaandalia chakula watu wasio na makao.