Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan afanya Mazungumzo na Putin kuhusu Mzozo wa Syria

Annan afanya Mazungumzo na Putin kuhusu Mzozo wa Syria

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Anna, amefanya mazungumzo na rais wa Urusi, Vladmir Putin mjini Moscow kuhusu mzozo wa Syria. Bwana Anna ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kuwa mzaungumzo yake na rais Putin yamekuwa mazuri sana, na kwamba yameangazia hatua zinazohitajika kuchukuliwa ili kukomesha ghasia na mauaji nchini Syria, na jinsi ya kwenda mbele na uundaji wa serikali ya mpito.

Ameongeza kuwa wameangazia pia majadiliano katika Baraza la Usalama kuhusu azimio jipya, na kuelezea matarajio yake Baraza hilo litaendelea na mjadala wake, na kufikia lugha ambayo itamvutia kila mmoja na kushirikiana kwenda mbele kuhusu mzozo huo.

“Kama nilivyosema awali, tunahitaji kufanya vyovyote vile kukomesha ghasia na mauaji. Nataraji kwamba Baraza la Usalama litatoa ujumbe kuwa mauaji ni lazima yakomeshwe, na kwamba hali iliyopo sasa Syria haikubaliki. Natumai kuwa Baraza litaungana na kuwa na ari moja ya kuendelea kutafuta amani”