Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Switzerland yaongoza kwa viwango vya ubunifu 2012

Switzerland yaongoza kwa viwango vya ubunifu 2012

Mpango wa kimataifa unaopima na kutoa viwango vya ubunifu umeitaja Switzerland kuwa ndiyo nchi inayoongoza kwa mwaka huu 2012, ikishika nafasi ya kwanza kwa ubunifu.

Kielelezo hicho cha ubunifu kilianzishwa na WIPO yaani shirika la kimataifa linaloangazia kazi za kitaaluma. Mara zote hutoa viwango kwa nchi 141 duniani ambazo zinatizamwa kuweka mipango mizuri ya kiubunifu katika maeneo ya kiuchumi.

WIPO kwa pamoja na chuo cha kimataifa cha masuala ya uchumi imetoa orodha ya nchi 10 zilizofanya vyema kwenye eneo hilo. Ukiweka kando Switzerland inayoshika nafasi ya kwanza, pia orodha hiyo kunakutikana nchi za Sweden, Singapore, Finland, Uingereza, Uholansi na, Denmark.

Pia zimo nchi za Hong Kong, Ireland na Marekani.Kwa kipindi cha miaka miwili sasa Switzerland imeendelea kushikilia nambari moja