Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka mafungamano zaidi ya kirafiki

Ban ataka mafungamano zaidi ya kirafiki

Kwenye siku ya kwanza ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya urafiki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon imeitolea mwito jamii ya kimataifa juu ya kile alichotaka ujenzi wa amani mpya ili kuleta ustawi wa maridhiano kwa dunia.Amesema kufikia shabaya ya kuwa na dunia yenye mafungamano ya mafanikio lazima kwanza wanajamii kutambua umuhimu wa kukaribisha urafiki na ujenzi wa amani mpya.

Katibu huyo Mkuu amesisitiza kuwa namna ilivyo muhimu kuendelea kuweka mshikamano wa pamoja hasa wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unapigania kufikia shabaya mbalimbali ikiwemo malengo ya maendeleo ya millenia .Alikumbusha makusudio yaliyomo kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa ambao pamoja na mambo mengine unasisitiza juu ya shabaya ya kueneza hali ya udugu na urafiki duniani kote.