Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban ataka Hollywood kuipiga jeki tuzo la Oscar kwa UM

KM Ban ataka Hollywood kuipiga jeki tuzo la Oscar kwa UM

Akitumia karata ya tuzo ya Oscar iliyotwaa Umoja wa Mataifa miaka 60 iliyopita kupitia filamu iliyoelezea hali ngumu za watoto wenye ulemavu, Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameanza kuishawishi Hollywood ili kukusanya fedha na hatimaye kuisambaza filamu hiyo duniani kote.

Filamu hiyo iliyotwaa tuzo ya Oscar mwaka 1947 iliyopewa jina la " hatua ya kwanza" ilijikita kumulika na kubainisha maisha jumla yanayowakabili watoto wenye ulemavu ambao wamesaulika kwa muda mrefu.

 

Lakini jambo kubwa zaidi filamu hiyo ililenga kuwakumbuka mamilioni ya watoto waliokabiliwa na matatizo ya ugonjwa wa polio ambao baadaye ulidhibitiwa kutokana na juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wahisani wake.

 

Kuhusu mafanikio hayo, Ban amesema kuwa ulimwengu unapaswa kufikiwa na ujumbe huo na ni muhimu kufanya hivyo kwani ulimwengu bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali.