Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mateso yaongezeka kwa raia nchini Syria:UNSMIS

Mateso yaongezeka kwa raia nchini Syria:UNSMIS

Mateso kwa raia wa Syria yanazidi kuongezeka wakati ghasia zikishika kasi nchini humo amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Syria UNSMIS , ikiwa ni siku chache tuu baada ya watu wa mpango huo kshambuliwa hali iliyofanya USMIS kusitisha shughuli zake.

Maja Jenerali Robert Mood akizungumza kwenye baraza la usalama amesema alifikia uamuzi huo wa ksitisha shughuli za uangalizi kutokana na hatari iliyopo na kutokana na ukweli kwamba hatari hiyo imefanya kuwa vigumu ktekeleza wajibu wao.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa UNSMIS wanafanya kazi katika mazingira magumu huku wakikabiliwa na ghasia na kulengwa ikiwemo makombora yanayovrmishwa na matukio mengine.

Amesema wakati huoho ameshuhdia mateso yanayowakabili wanawake, waname na watoto wa Syria huku wengine wakiwa wamekwama kwenye mapigano ambayo sasa yamefikia hali mbaya zaidi.