Njia mpya yapatikana kufuatilia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

6 Juni 2012

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amezindua Jumanne Mkakati wa pamoja wa Utekelezaji au IIF, ambao ni mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka kumbukumbu na kufuatilia ahadi zilizotolewa na jumuiya ya kimataifa katika kufikia malengo haya.

Bwana Ban amesema kuwa tovuti la IIF ni mpango muafaka wa kimataifa wa kufuatilia mkutano mkuu wa MDGs wa 2010 na wajibu wa Baraza Kuu kuripoti kuhusu mafanikio yanayopatikana katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia yaani Malengo ya Milenia ya Milenia (MDGs).

"Tovuti ya IIF labda ni kazi ndogo ya kubonyeza kwa mtumiaji wa computa –- lakini ni maendeleo makubwa katika jitihada zetu za kuongeza uwajibikaji ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya milenia. Wakati umefika. Mataifa wanachama wametoa ahadi nyingi za kusaidia utekelezaji wa MDGs, hata hivyo hatujapata mafanikio katika pande zote.