Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumekuwa Tukiwaangusha Vijana wetu wa Kike na wa Kiume:ILO

Tumekuwa Tukiwaangusha Vijana wetu wa Kike na wa Kiume:ILO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani anayemaliza muda wake Juan Somavia amesema dunia imekuwa ikiwangusha vijana wake wa kike na wa kiume kwa muda sasa.

Akizungumza kwenye mkutano wa ILO Jumatano bwana Somavia amesema kwa ujumla kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana ni karibu mara tatu ya kile cha watu wazima, na zaidi ya hapo wale wanaopata ajira wengi hufanya kazi kwa saa chache, mikataba ya muda, katika sekta zisizo rasmi au kazi zisizo za maana.

Somavia amesema kuna maingiliano madogo sana pale watu wazima ambao wanaunda sera na kuwafanya vijana kubeba mzigo mkubwa wa matatizo yanayoikabili dunia hivi sasa ikiwemo ajira. Na vijana wengi hawataki kukubali mustakhbali wao bila ajira, kazi duni, elimu duni na masuala mengine.

(SAUTI YA JUAN SOMAVIA)