Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bank ya dunia imezitaka serikali kufikiria masuala ya mazingira zinapokuza Uchumi

Bank ya dunia imezitaka serikali kufikiria masuala ya mazingira zinapokuza Uchumi

Bank ya dunia Jumatano imetoa ripoti ikizitaka serikali duniani kufikiria masuala ya mazingira zinapojitahidi kutunga sera za ukuzaji uchumi ambazo zitajumuisha wote, zinazotekelezeka, zilizo na gharama nafuu na zaidi ya yote, zitakazokuwa za umuhimu kuhakikisha uchumi unakuwa kila mwaka.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa kwenye mkutano wa kimataifa wa ukuaji unaojali mazingira mjini Seoul umebainisha mikakati ambayo ni muhimu kuzingatia ikiwemo hali ya hewa, ardhi na mfumo wa masuala ya baharini, kwamba inahitajika ili kupunguza umasikini.

Ripoti hiyo pia imeelezea mtazamo walionao wengi kwamba uchumi unaojali mazingira ni ufahari ambao nchi nyingi haziwezi kumudu, na badala yake imetaja vikwazo vya kisiasa, tabia na baadhi ya nchi na masala ya ufadhili wa fedha kuwa ndio matatizo na sio uchumi unaojali mazingira.

Ripoti imetoa changamoto kwa serikali kubadili mitazamo yao kuhusu sera za ukuaji wa uchumi, kuweka vipimo sio tu kwa wanayozalisha bali pia kwa vinavyotumika na kuchafua mazingira katika mchakato mzima. Serikali ya Korea imeahidi kutoa dola milioni 40 ili kuimarisha na kupanua wigo wa benki zinazozingatia masuala ya mazingira duniani kote.