Mpango wa amani wa Syria bado unaendelea:Annan

4 Mei 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu Kofi Annan amesema kuwa mpango wa amani wa Syria unaendelea hata kama kumekuwa na ripoti za ukiukaji kwenye maafikiano ya kusitisha ghasia.

Annan amesema kuwa hata kama hakuna dalili za kutekelezwa kwa yaliyoafikiwa kwenye mpango huo wa amani kuna dalili kidogo hata baada ya kuondolewa kwa silaha znito kutoka kwa maeneo ya raia. Annan amesema kuwa hali iliyopo nchini Syria imeendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita na haitachukua siku moja au juma moja kuisuluhisha. Ahmad Fawzi ni msemaji wa Annan.

(SAUTI YA AHMAD FAWZI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter