Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Coomaraswamy aelezea wasiwasi wa mashambulizi nchini Syria

Coomaraswamy aelezea wasiwasi wa mashambulizi nchini Syria

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy ameelezea wasi wasi wake kufuatia misururu ya mauaji na kujeruhiwa kwa watoto nchini Syria ya ripoti kusema kuwa watoto wawili waliuawa hii leo kwenye shambulizi la bomu. Tangu kutekelezwa kwa makubaliano ya tarehe 12 mwezi Aprili kati ya serikali ya Syria na upinzani na hata baada ya kutumwa kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifakwenda nchini Syria zaidi ya watoto 34 wameripotiwa kuuawa nchini Syria.

Mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyoikumba miji ya Damascus na Idlib yalisababisha maaafa zaidi miongoni mwa watoto. Mashambuzli hayo yamevuruga usalama nchini Syra na kuyaweka maisha ya watoto hatarini.