Ban na Quartet washutumu mauaji ya raia Gaza

Ban na Quartet washutumu mauaji ya raia Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiungana tume maalumu ya kusaka amani mashariki ya kati Quartet wote kwa pamoja wameshutumu vikali tukio la kuuwawa kwa familia moja ya Kisrael iliyouwawa katika eneo la ukingo wa gaza, mwishoni mwa juma.

Familia hiyo ya watu watano wakiwemo watato watatu, waliuwawa na watu wasiojulikana katika eneo walilokuwa wakiishi karibu na kijiji cha Nablus pale mhusika alipoivamia nyumba yao na kutekeleza shambulio hilo.

Ban ametaka pande zote kujizua na matikio ya jabza ili kukaribisha duru ya maelewano. Tume ya kidiplomasia inayozingatia eneo hilo Quartet inahusika pande kadhaa ikiwmo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani.

Pande zote zimezungumia mauaji hayo na kutaka wahusika wake kufikishwa mbele ya sheria na wakati huo huo imepongeza taarifa iliyotolewa na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas aliyeyalaani mashambulizi hayo.