Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wenye viwango vya juu vya joto:WMO

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wenye viwango vya juu vya joto:WMO

Ripoti ya kila mwaka ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kuhusu hali ya hewa inasema kuwa mwaka 2011 uliandikisha viwango vya juu zaidi vya joto na ni mwaka wa 11 kati ya miaka yenye viwango vya joto vya juu zaidi tangu takwimu hizo zianze kuchukuliwa mwaka 1850.

Hali hii ilizua athari tofauti duniani yakiwemo mafuriko yaliyotokea kwenye mabara yote duniani na kiangazi kilichoshuhudiwa eneo la Afrika Mashariki na Marekani pamoja tufani mbaya nchini marekani.

Kando na hilo WMO pia ilitangaza matokeo yanayoonyesha kuwa kulishudiwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kati ya mwaka 2001- 2010 ambao ndio mwongo wenye viwango vya juu zaidi vya joto kuwai kushuhudiwa.