Mkataba wa UNECE waadhimisha miaka 20 tangu kutiwa sahihi

16 Machi 2012

Makubaliano ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa ya ulaya kuhusu utunzaji na matumizi ya maji na maziwa ya kimataifa UNECE yaliyoafikiwa mjini Helsinki Finland machi 17 mwaka 1992 hii leo yameadhimisha miaka 20 tangu yatiwe sahihi.

Tangu kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo bara la Ulaya limepiga hatua kubwa katika masuala ya ushirikiano kwenye mipaka ya maji.

Hadi sasa karibu mataifa yote katika eneo hilo yamechukua hatua za  kufanya ushirikiano kwa maji yaliyo kati ya nchi zao.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter