Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa mwongozo wa kuzuia ukwepaji ushuru

UM watoa mwongozo wa kuzuia ukwepaji ushuru

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba umetoa mwongozo mpya wa kuzuia ulipaji ushuru mara mbili kati ya nchi na pia katika kuzuia wanaokwepa kulipa ushuru suala ambalo linagharimu nchi dola trillion tatu kila mwaka.

Mikataba ya ulipaji ushuru mara mbili ni makubaliano kati ya serikali ya kuzuia watu kulipa ushuru mara mbili kati ya nchi mbili. Mikataba kama hii huwa yenye manufaa kubwa katika kuchangia uwekezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya wataalamu wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu masuala ya ushuru Lara Yaffar amesema kuwa lengo ni kuziwezesha nchi zinazoendelea kuingia kwenye makubaliano haya kwa manufaa ya maendeleo.