Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua kali na sera dhaifu zinaathiri ufufuaji wa uchumi

Hatua kali na sera dhaifu zinaathiri ufufuaji wa uchumi

Hatua kali, sera dhaifu na ukosefu wa ajira vimeelezewa kutia dosari juhudi za kupunguza umasikini na kufufua uchumi uliokumbwa na mdororo mkubwa na kuchagiza maendeleo endelevu yanayojali mazingira.

Hayo yameelezwa wakati wa kuhitimisha mkutano wa kimataifa wa baraza la chumi na jamii ECOSOC uliojumuisha taasisi za uchumi na biashara.

Jomo Kwame Sundaram katibu mkuu msaidizi wa masuala ya uchumi na maendeleo ameonya kwamba utekelezaji wa sheria kali unaweza weka hatarini juhudi za ufufuaji wa uchumi hasa wakati huu ambapo nchi nyingi zinahitaji sio tuu kufufua uchumi bali kuaminiwa tena na wananchi wake.

(SAUTI YA JOMO KWAME SUNDARAM)