Radio ni daraja la mawasiliano kwa mamilioni ya watu

17 Februari 2012

Kwa mara ya kwanza wiki hii dunia imeadhimisha siku ya Radio duniani, ikienda sambamba na miaka 66 tangu kuanzishwa Radio ya Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO liliamua kuitenga Februari 13 kuwa siku ya Radio duniani kwa lengo la kusherehekea mchango wa Radio, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa miongoni mwa Radio na kuwachagiza wafanya maamuzi kuanzisha na kutoa fursa ya watu kupata taarifa kupitia Radio zikiwemo Radio za jamii.

Kwa mujibu wa mkrugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova Radio ina umuhimu wa pekee duniani, ni daraja la kufikisha habari na taarifa kwa watu wengi zaidi kuliko njia zingine za mawasiliano. Flora Nducha ameandaa makala hii.

(MAONI YA WATU)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud