Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa ECOSOC waanza mjini New York

Mkutano wa ECOSOC waanza mjini New York

Kuangamiza umaskini na ajira kwa vijana yatakuwa kati ya masuala yatayoangaziwa kwenye mkutano wa 50 wa tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na maendeleo ya kijamii ambao unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Kwa muda wa siku kumi zijazo tume hiyo itafanya vikao kadhaa jinsi ya kufanyia mabadiliko sera kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya jamii hasa changamoto za kisasa zikiwemo hali mbaya ya uchumi duniani na mabadiliko ya hali ya hewa.

Tume hiyo pia itaangazia zaidi changamoto zinazowakumba vijana hasa za kupata ajira baada ya makadirio ya Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwa vijana wanakosa ajira mara tatu zaidi kuliko watu wazima.