Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito wa uhamasishaji na kutimiza ahadi za haki za wanawake watolewa:Bachelet

Wito wa uhamasishaji na kutimiza ahadi za haki za wanawake watolewa:Bachelet

Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake yaani UN Women Bi Michelle Bachelet ametoa wito wa dunia kutimiza ahadi na kuchukua hatua kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa wanawake wakati huu ambapo siasa na hali ya uchumi inatishia maendeleo ya haki za wanawake.

Akizungumza katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuundwa kwa UN Women Bachelet amesema wakati hatua kali zinachukuliwa , kupunguza bajeti na mabadiliko ya kisiasa vinaathiri maisha ya wanawake duniani kote.

Pia ameainisha ajenda zitakazopewa kipaumbele na chombo hicho kwa mwaka 2012 kuwa ni kurejea kutoa msukumo wa kuwawezesha wanawake kiuchumi na ushiriki wao katika siasa. Amesema hii ni kutokana na madai ya wanawake, matukio ya hivi karibuni na pia mabadiliko yanayojitokeza katika Nyanja ya siasa, kijamii na kiuchumi.

(SAUTI YA MICHELE BACHELET)