Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa mkesha wa kuzuru Chernobly Ban aainisha njia za kuimarisha usalama wa nyuklia duniani

Wakati wa mkesha wa kuzuru Chernobly Ban aainisha njia za kuimarisha usalama wa nyuklia duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa dunia kuhakikisha nishati ya nyuklia inatumika kwa amani na usalama.

Akizungumza mjini Kiev Ukraine kwenye mkutano wa usalama wa matumizi ya nishati ya nyuklia Ban amelinganisha zahma ya nyuklia ya Chernoby miaka 25 iliyopita na na tafrani ya Fukushima Daiichi Japan mwaka huu.

Amesema matatizo yote hayo mawili yanatishia afya ya binadamu na mazingira , yanasababisha matatizo ya kiuchumi na kuathiri kila kitu kuanzia kilimo, biashara na huduma za kimataifa.

Amebainisha hatua tano za kuhakikisha usalama wa nyuklia siku za usoni ikiwa ni pamoja na haja ya kuimarisha ushirikiano na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA kuhusu changamoto za usalama wa nyuklia, haja ya viwango vya kimataifa katika ujenzi wa mitambo, kukubaliana kuhakikisha usalama wa jamii, uwazi na kushirikiana taarifa miongoni mwa mataifa na umuhimu wa kujenga na kuandaa mitambo ya nyuklia kukabiliana na majanga kama tetemeko, tsunami , moto na mafuriko.

Amesema ni uchungu mkubwa kupatwa na zahma ya nyuklia lakini pia ni funzo kwa wote.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)