Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka uchunguzi wa ajali ya meli Italia ufanyike

UM wataka uchunguzi wa ajali ya meli Italia ufanyike

Uchunguzi wa kina wa jinsi gani meli ya abiria ilivyopinduka kwenye mwambao wa Italia wapaswa kufanyika amesema afisa wa Umoja wa Mataifa.

Duru za habari zinasema watu sita wameaarifiwa kufa maji na wengine 16 hawajulikani walipo baada ya chunga la meli kufuunuka. Jumla ya abiria 4200 na mabaharia walikuwa ndani ya meli hiyo .

Katibu Mkuu wa shirika la kimataifa ubaharia IMO Koji Sekimiz amesema inaweza kuwa ni muhimu kupitia upya sheria za usalama wa meli kubwa za abiria , lakini itategemeana na matokeo ya uchunguzi.

IMO yenye makao yake makuu London ni shirika la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kuangalia usalama wa masuala ya usafiri wa meli.