Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa kwanza wenye misaada wakaribia Jonglei

Msafara wa kwanza wenye misaada wakaribia Jonglei

Msafara wa kwanza wa malori na magari mengine yakiwa na shehena za misaada kwa ajili ya huduma mbalimbali unakaribia kuwasili katika jimbo la Jonglei Sudan Kusin ambalo katika siku za hivi karibuni limeshuhudiwa likiandamwa na mapigano ya kikabila.

Watu zaidi ya 7,500 wanaripotiwa kuathiriwa na machafuko hayo ambayo yanahusisha makabila ya sehemu mbili.

Msafara huo unaoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, umebeba vifaa mbalimbali ikiwemo vile vya kuokolea maisha na kukithi mahitaji mengine.

Pia helkota ambayo itabeba huduma nyingine mbalimbali inatarajiwa kuelekea katika mji wa Pibor ambako ndioko chimbuko la machuko hayo .

Msafara huo wa kwanza ambao unaungwa mkono na serikali ya Sudan Kusin unatazamiwa kuwasili katika mji wa Pibor siku ya jumamosi.