Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto warejea shuleni nchini Libya

Watoto warejea shuleni nchini Libya

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 1.2 nchini Libya wamerejea shuleni. Masomo nchini Libya yalivurugwa na mapigano yaliyosababisha kuondolewa madarakani kwa rais Muammar Qhadafi mwaka uliopita.

Msemaji wa UNICEF Marixie Mercado amelitaja suala la kurejea shuleni kwa watoto hao kama mafanikio makubwa ya kurudi kwa hali ya kawaida kwa maisha ya watoto nchini Libya.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)