Ufadhili kutoka UM kuwasaidia wakulima nchini Lesotho

Ufadhili kutoka UM kuwasaidia wakulima nchini Lesotho

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuboresha maisha ya watu maskini wanaoishi vijijini linatoa dola milioni 10 ili kuwasaidia wakulima wadogo nchini Lesotho kuboreshaa kilimo.

Kwenye makubaliano yaliyotiwa sahihi mjini Rome mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na serikali ya Lesotho yana lengo la kuwasaidia wakulima wadogo kuboresha uzalishaji kwenye wilaya 4 kati ya wilaya 10 ndogo nchini humo. Kulingana na IFAD zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wa Lesotho wanaishi vijijini ambapo idadi kubwa wanahusika na kilimo.