Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati ya kuachana na taa zisizofaa yatangazwa:UNEP

Mikakati ya kuachana na taa zisizofaa yatangazwa:UNEP

Serikali ya Afrika ya Kusini ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban (Cop 17) Jumatano imetangaza rasmi mipango ya sera za kitaifa za kuachana na matumizi ya taa zisizojitosheleza.

Mpango huo una maingiliano na mkakati wa kimataifa wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP unaoungwa mkono na kitengo cha mazingiro cha kimataifa GEF ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuhamia matumizi ya nishati ya taa zinazojali mazingira. Afrika ya Kusini itakuwa taifa la kwanza barani Afrika kuingia katika awamu hiyo ya kuachana na matumizi ya taa zisizojitosheleza katika uhifadhi wa mazingira.

Kwa mujibu wa UNEP mabadiliko hayo ni kitu rahisi, cha haraka na cha gharama nafuu katika kuhifadhi nishati na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewaia . Nishati ya umeme kwa ajili ya kuwasha taa ni asilimia 20 ya umeme wote unaozalishwa duniani na ni asilimia 6 ya gesi yote ya viwandani.

Ushirikiano wa kimataifa wa UNEP/GEF unazima taa zote za zamani na kuingia katika njia mpya ya taa ambayo inazalisha gesi ndogo sana ya cabon. Lengo ni kuhakikisha ifikapo mwka 2016 mabadiliko hayo sio tuu yanawezekana bali yanafanyika amesema mkurugenzi mkuu wa UNEP Achim Steiner.

Mpango wa UNEP/GEF ulizinduliwa rasmi mwaka 2009 kama juhudi za kimataifa za kuchagiza matumizi ya taa muafaka za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.